Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
amesema ataanzisha uchunguzi kuhusiana na shambulio katika majengo ya
umoja huo hivi karibuni katika mashambulizi ya Gaza.
Bw. Ban Ki-moon amesema uchunguzi
huru utaangalia matukio mabaya zaidi ambayo yalisababisha vifo vya
watu wasio na hatia.
Bw. Ki-moon amesema uchunguzi huo
pia utafanya tathimini taarifa za kutumika kwa majengo ya Umoja wa
Mataifa kuhifadhi silaha.
Mgogoro huo wa Gaza uliodumu kwa
siku 50, ulisababisha vifo vya Wapalestina 2,100 na Waisraeli 73.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni