Daktari wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC), ameshinda tuzo ya juu ya Haki za Binadamu Ulaya kwa
kuwasaidia maelfu ya waathirika wa matukio ya kubakwa na watu wengi
nchini kwake.
Daktari huyo Denis Mukwege
alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya Sakharov na bunge la Ulaya huko
Strasbourg, ambayo inaendana na zawadi ya dola elfu 63.
Daktari huyo wa wanawake alianzisha
Hospitali ya Pazi, mashariki mwa Congo mwaka 1999 ili kuwatibu
wanawake ambao wamekumbwa na matukio ya kutisha ya kubakwa.
Miaka miwili iliyopita Dk. Mukwege
alinusurika kuuwawa kwa kutuhumu kuendelea kwa ukatili wa kingono
nchini DRC unaofanywa na vikosi vinavyopigana kumiliki eneo lenye
utajiri wa madini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni