Usalama umeimarishwa hii leo huko
Mombasa Kenya wakati ambapo mamia ya waombolezaji wakiuaga mwili wa
mwanazuoni maarufu Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla marehemu
Prof. Al-Amin Mazrui anayezikwa leo.
Mwili wa Profesa huyo wa sayansi ya
siasa, aliyefariki dunia Oktoba 13 nchini Marekani umewasili leo
majira ya saa tisa usiku, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi,
na kupelekwa kwenye nyumba yake iliyopo Old Town karibu na Fort
Jesus.
Miongoni mwa watu waliokuwepo
kuulaki mwili wa Prof. Mazrui ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Kenya
Willy Mutunga, aliyekuwa Kadhi mkuu Sheikh Hamad Kassim pamoja na
Gavana wa Mombasa Hassan Joho, pamoja na ndugu na jamaa wa karibu wa
marehemu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni