.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 19 Oktoba 2014

HOFU YA EBOLA YAWAFANYA BAADHI YA WAKAZI WA OKLAHOMA KUWAHOFIA YATIMA KUTOKA KENYA

Kundi la yatima kutoka Kenya waliokatika safari nchini Marekiani wanakabiliwa na pingamizi la baadhi ya wakazi wa Oklahoma ambao wanaamini kuwa watoto hao wanamaambukizi ya virusi vya Ebola.

Hata hivyo wadhamini na wenyeji wa watoto hao 24 wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kisumu, wamepinga vikali hoja hiyo ya kuwahusisha yatima hao na ugonjwa wa Ebola.

Tangu watoto hao wafike Marekani wiki iliyopita kumekuwa na hofu kwa idadi ndogo ya wakazi wa Oklahoman, kuwa huenda wakawa na maambukizi ya virusi vya Ebola, hii imechangiwa na wakazi hao kuto jua Jografia ya Afrika.

Mwanzilishi wa Kituo hicho cha Yatima Beatrice Atieno Williamson, ameliambi gazeti Oklahoma kuwa mlipuko wa Ebola upo katika nchi za Afrika Magharibi, wakati watoto hao yatima wametokea Kenya ambayo ipo Afrika Mashariki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni