Vikosi vinavyoongozwa na Marekani
vimeongeza mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa kundi la IS,
wanaotishia mji wa Kobane nchini Syria ulipo karibu na mpaka na
Uturuki.
Muungano huo umeendesha mashambulizi
ya anga 21 katika siku mbili na kusaidia kuwadhibiti wapiganaji wa IS
wasisonge mbele.
Rais Barack Obama amebashiri
uwezekano wa kuwepo kwa kampeni ya muda mrefu dhidi ya kundi la IS
linaloshikilia maeneo makubwa katika nchi za Syria na Irak.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni