Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius anarejea mahakamani hii leo katika muendelezo wa siku ya
tatu ya kusikiliza maelezo kabla ya kujua hatma yake iwapo atafungwa
jela kwa kumuua mpenzi wake.
Siku ya jumanne mwendesha mashtaka
alisema familia ya Reeva Steenkamp, ilikataa ofa ya fedha alizoziita
fedha za damu kutoka kwa Pistorius.
Hata hivyo wakili wa familia ya
Steenkamp amesema kuwa wamekuwa wakipokea malipo ya kila mwezi kutoka
kwa Pistorius kwa miezi 18 sasa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni