Polisi Hong Kong wamepambana na
waandamanaji wanaodai Demokrasia, wakati wakijaribu kusafisha njia
karibu na makao makuu ya serikali.
Mamia ya maafisa polisi waliovaa
mavazi ya kukabiliana na ghasia walipuliza hewa ya vumbi ya pilipili
katika kuwasambaza waandamanaji, na kukamata makumi ya watu.
Polisi wamesema barabara ya Lung Wo
ilipaswa kusafishwa kwa kuwaondoa waandamanaji kwa kuwa ni njia kuu
muhimu.
Baada ya mapambano hayo, polisi
wamesema maafisa wake waliohusika katika kuwapiga waandamanaji,
watahamishwa vitengo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni