Waandamanaji waliokerwa na mipango
ya kumruhusu rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore kuongeza muda wake
wa utawala wa miaka 27, wamechoma moto bunge.
Mashuhuda wamesema katika Jiji la
Ouagadougou, jengo la Jiji na Makao Makuu ya chama tawala pia nayo
yamechomwa moto.
Vikosi vya ulinzi vimerusha mabomu
ya machozi kutoka kwenye helkopta, wakati kundi la watu likielekea
makazi ya rais.
Wabunge wamesitisha zoezi la upigaji
kura ya kuridhia rais Compaore kuwania tena kiti cha urais katika
uchaguzi mkuu.
Waandamanaji wenye hasira wakionyesha hasira zao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni