.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 30 Oktoba 2014

RUBANI ASHUSHWA NA KUFUNGULIWA MASHITAKA MUDA MFUPI KABLA YA KURUSHA NDEGE BAADA YA KUGUNDULIKA KUWA AMELEWA

 Rubani mmoja wa ndege ya shirika la ndege la Flybe alijukuta akiangukia mikononi mwa polisi muda mfupi kabla ya kurusha ndege baada ya kubainika kuwa alikuwa amelewa. 

Rubani huyo alikuwa airushe ndege hiyo kutoka uwanja wa ndege wa Newquay kuelekea London Gatwick, kabla ya wasaidizi wake kutoa taarifa polisi kuwa amelewa chakari, hali iliyowalazimu polisi kumshusha na kwenda kumfanyia kipimo cha ulevi na kumfungulia mashitaka.

Kufuatia tafrani hiyo iliyotokea jumatano, safari ya ndege hiyo ilifutwa kwa muda hali iliyosababisha abiria waliokuwa wanasafiri na ndege hiyo kuchelewa kuunganisha ndege nyingine kuendelea na safari zao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni