.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

WAZIRI MKUU MH MIZENGO PINDA AKIWA ZIARANI NCHINI POLAND

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watanzania waishio Poland baada ya kuwasili jijini Warsaw kwa ziara ya kikazi Oktoba 24, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Poland jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Poland jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. Wengine Pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland, Bw. Marek Kloczko,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Polland, (Under Secretary Of State Ministry of Foreign Affairs), Bibi Katarzyna Kacperczyk na Bwana Jerzy Pietrewiez ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi ya Polland.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Poland wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia jijini Warsaw Oktoba 24, 2014.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua matrekta yanayotengenezwa katika kiwanda cha ROL- BRAT kilichopo Warsaw, Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014.
Waziri Muu, Mizengo Pindaakipata maelezo kutoka kwa mshauri wa uchumi nchini Polland Bw, Aleksandr Zincman(kushoto) kuhusu usindikaji ngano wakati alipokagua kiwanda cha kusindika unga cha Chojnow nchini Polland akiwa kayika ziara ya kikazi nchini huo Oktoba 24, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mshauri wa uchumi nchini Polland Bw, Aleksandr Zincman (kulia) wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza maghala ya kuhifadhia nafaka (silos), mashine za kukausha nafaka na mashine za kusafisha nafaka cha Chojnow nchini Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. 

                                                                                 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni