Waziri wa Viwanda na Biashara Yuko
Obuchi amejiuzulu kufuatia madai kuwa alitumia vibaya fedha za
shughuli za kisiasa, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni pigo kwa Waziri
Mkuu Shinzo Abe.
Waziri huyo Yuko Obuchi anadaiwa
kutumia fedha za kundi lake la kisiasa pamoja na michango mingine
katika kununua vipodozi pamoja vitu visivyohusiana na siasa.
Waziri Obuchi amewasilisha barua
yake ya kujiuzulu kwa Bw. Abe katika mkutano wao uliodumu kwa dakika
30.
Wachambuzi wa mambo wanasema
kujiuzulu kwa Obuchi kunadhohofisha jitihada za Bw. Abe za kuwapatia
nafasi za uongozi wa juu wanawake zaidi.
Waziri Abe ameshapoteza mawaziri wawili wanawake kati ya watano aliowateuwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni