Rais wa Liberia Ellen Johnson
Sirleaf amesema dunia nzima inawajibika katika mapambano dhidi ya
ugonjwa hatari wa Ebola.
Katika barua yake kwa dunia
iliyorushwa na kituo cha BBC, amesema ugonjwa huo haujali mipaka na
kila nchi zinapaswa kuwajipika katika kupambana nao.
Rais Johnson Sirleaf ameongeza kuwa
kizazi cha Afrika kipokwenye hatari ya kupotelea kwenye janga la
kiuchumi.
Mlipuko wa Ebola umeuwa zaidi ya
watu 4,500 katika nchi za Afrika Magharibi, wakiwemo 2,200 nchini
Liberia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni