.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

WELBECK APIGA GOLI 3 WAKATI ARSENAL IKIIFUNGA GALATASARAY 4-1 LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mshambuliaji wa Arsenal mwenye kasi zaidi uwanjani Danny Welbeck jana usiku aliibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray iliyosafiri kutoka nchini Uturuki katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya. 

Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Emirate jijini London. Welbeck aliifungia Arsenal mabao matatu katika dakika za 22, 30 na 52 huku bao la nne likifungwa na Alexis Sanchezi katika dakika ya 40 mchezo huo. 

Bao la kufutia machozi la Galatasaray lilifungwa kwa penati na Yilmaz baada ya mlinda mlango wa Arsenal, Wojciech Szczesny kumwangusha katika eneo la hatari mchezaji huyo.
Mlinda mlango wa Arsenal, Wojciech Szczesny akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha mshambuliaji wa Galatasaray, Buark Yilmaz katika eneo la hatari.

Mashabiki wa Galatasaray wakiwasha fataki wakati timu yao ilipokuwa ikicheza na Arsenal jana usiku katika mchezo huo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni