.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 14 Novemba 2014

BIBI KIZEE WA MIAKA 91 AZINDUKA AKIWA MOCHWARI BAADA YA KUDAIWA KUFA

Bibi mwenye umri wa miaka 91 amewashangaza wafanyakazi wa chumba cha maiti Jijini Warsaw nchini Poland baada ya kuzinduka akiwa ndani ya mfuko wa kuhifadhia maiti saa kumi na moja kupita tangu alipotangazwa kuwa amefariki duni nyumbani kwake.

Televisheni ya nchi hiyo imemtaja bibi huyo kuwa ni Janina Kolkiewicz ambaye aliinuka akiwa ndani ya mfuko wa kuhifadhia maiti katika chumba cha maiti chenye ubaridi mashariki mwa Poland hapo jana.

Daktari Wieslawa Czyz aliyethibitisha kifo hicho aliiambia Televisheni hiyo kuwa alikuwa na uhakika kuwa bibi huyo alikuwa amekufa na kuongeza kuwa ameshangazwa na kuwa haelewi kilichotokea kwani moyo wake ulisimama na alikuwa hapumui, polisi imeanza uchunguzi wa tukio hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni