.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 27 Novemba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, ARSENAL YAIADABISHA BORUSSIA DORTMUND

Mshambuliaji mahiri wa Arsenal, Alexi's Sanchez akiifungia timu yake bao la pili. 

Wakicheza nyumbani katika uwanja wao wa Emirates, washika bunduki wa London, Arsenal usiku wa kuamkia leo wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund toka Ujerumani katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya.
 Katika mchezo huo, Arsenal walijipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Yaya Sanogo katika dakika ya pili ya mchezo, bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Arsenal kujipatia bao la pili kupitia kwa Alexi's Sanchez katika dakika dakika ya 57 na kuamsha furaha kwa mashabiki wa Arsenal ambao walikuwa wakiishangilia timu yao mwanzo mwisho.
Sanogo akiifungia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 2 ya mchezo huo dhidi ya Borussia Dortmund usiku wa kuamkia leo. 

Matokeo mengine ya michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ni kama ifuatavyo:-

Atletico Madrid 4 vs 0 Olympiakos

Malmo FF 0 vs 2 Juventus

Ludo 2 vs 2 Liverpool

Zenit 1 vs 0 Benfica

Bayer 04 Leverkusen 0 vs 1 Monaco
 
Anderlecht 2 vs 0 Galatasaray 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni