.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, MANCHESTER CITY YAUONA MWEZI YAIFUNGA BAYERN MUNICH 3-2

Timu ya soka ya Manchester City wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad, usiku wa kuamkia leo wamewaduwaza vinara wa ligi kuu nchini Ujerumani, Bayern Munich baada ya kuwatandika mabao 3-2 katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, mchezo amabao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu.
Manchester City ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati, mfungaji akiwa ni Aguero kunako dakika ya 21. Hata hivyo Bayern Munich walizinduka na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 40 mfungaji akiwa ni Alonso huku mshambuliaji mahiri Lewandowski akiifungia Bayern bao la pili katika dakika ya 45 ya mchezo huo.
Bayern Munich wakionekana kama ndio wanaondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo, kibao kiligeuka katika dakika ya 85 pale Aguero alipoifungia Man City bao la pili na pia kurejea tena nyavuni katika dakika ya 90 kuifungia timu yake bao la 3 nala ushindi. 

Hadi mwisho wa mchezo huo, Manchester Cty 3 na Bayern Munich 2. Pamoja na matokeo hayo, Bayern Munich wanaongoza kundi wakiwa na pointi 12, Roma wapo nafasi ya pili na pointi 5, CSKA Moscow wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 5 na Manchester City wapo mkiani wakiwa na pointi 5 ila wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni