.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Novemba 2014

LIONEL MESSI AFIKIA REKODI YA MAGOLI NA KUWEKA REKODI MPYA LA LIGA

Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi amekuwa mwanasoka wa Ligi Kuu ya Hispania anayeoongoza kwa kufunga magoli mengi katika ligi hiyo maarufu kama La Liga baada ya kufunga mabao matatu hat-trick dhidi ya Sevilla.

Lionel Messi amefikia rekodi ya magoli 251 iliyowekwa na Telmo Zarra, kwa kufunga goli tamu la mpira wa adhabu, baada ya kushindwa kufunga katika michezo mitatu iliyopita ya La Liga.

Katika mchezo huo na Sevilla ilisawazisha bao hilo kupitia goli la kujifunga la Jordi Alba, kabla ya Neymar kuifungia Barcelona bao la pili.

Nae Ivan Rakitic naye alifunga bao lake kwa kichwa, kabla ya Messi kucheka tena na wavu na kuweka rekodi mpya ya magoli 253 kufuatia gonga baina yake na Mbrazil Neymar na hadi mwisho Barcelona 5 Sevilla 1.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni