.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

MAKAMU WA RAIS ZIMBABWE ANG'OLEWA MADARAKA NDANI YA CHAMA TAWALA

                          Makamu wa Rais Joice kushoto akiwa na rais Robert Mugabe
 
Makamu wa rais wa Zimbabwe ameng'olewa madaraka katika chama tawala, kufuatia kampeni iliyofanywa na mke wa Rais Robert Mugabe, Grace huku kukiwa na mvutano wa nani atamrithi Mugabe ukipamba moto.

Makamu huyo Joice Mujuru amejikuta akishambuliwa na Grace Mugabe, aliyedai kuwa makamu huyo wa rais anachukua fedha kwenye kampuni na kuunda makundi yanayotishia kukipasua chama tawala cha ZANU-PF.

Bi. Mujuru anatuhumiwa kupanga njama za kumuua rais Mugabe, wakati watu katika chama hicho wakipambana kutafuta kurithi nafasi ya urais pindi atakapoondoka madarakani rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90 ama atakapofariki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni