Mchezaji kriketi wa Australia Phil
Hughes amefariki dunia hospitali ikiwa imepita siku mbili baada ya
kupigwa kichwani na mpira wakati wa mchezo uliofanyika Sydney.
Mkuu wa Timu ya Madaktari wa
Australia, Dk. Peter Brukner amesema mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 25, hakurejewa na fahamu tangu apatwe na tukio hilo.
Hughes, ambaye pia alichezea timu za
Hampshire, Middlesex pamoja na Worcestershire, alipigwa kichwani na
mpira wa karibu uliopigwa na Sean Abbott.
Tukio lenyewe lilikuwa hivi..hapa mpira ukimpiga kichwani
Phil Hughes akianguka chini baada ya kupigwa na mpira huo
Tukio lenyewe lilikuwa hivi..hapa mpira ukimpiga kichwani
Phil Hughes akianguka chini baada ya kupigwa na mpira huo
Bowler Sean Abbott aliyempiga na mpira Hughes akitoka hospitali akiwa na huzuni baada ya kupewa habari ya kifo.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni