.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 27 Novemba 2014

MISIKITI ILIYOFUNGWA NA SERIKALI MOMBASA YAFUNGULIWA CHINI YA ULINZI MKALI

Wakazi wa eneo la Majengo Mombasa Kenya sasa wanaweza kuingia kwenye misikiti iliyofungwa, baada ya makubaliano baina ya serikali, wanataaluma na viongozi wa Kiislamu ya kufunguliwa kwa misikiti hiyo.

Kumekuwepo na ulinzi mkali katika mji huo wakati msikiti wa Masjid Musa ulipofunguliwa mapema leo.

Makumi ya watu walikusanyika kushuhudiwa kufunguliwa kwa msikiti huo wakati vijana wakichukua majukumu ya kuusafisha msikiti huo pamoja na mazingira yake.

Misikiti mingine ya Sakina, Minaa na Swafaa nayo pia ilikuwa inatarajiwa kufunguliwa hii leo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni