Afisa polisi wa
Marekani Darren Wilson aliyempia risasi na kumuua kijana mweusi asiye
na silaha Michael Brown huko Missouri katika Mji wa Ferguson
amejiuzulu wadhifa wake, wakili wake Neil Bruntrager amesema.
Wakili Bruntrager
ameviambia vyombo vya habari nchini Marekani uamuzi huo wa mteja wake
kujiuzulu wadhifa polisi umeanza mara moja.
Polisi huyo Wilson
amenukuliwa akisema amechukua uamuzi huo kutokana na tishio la
kuendelea kwa ghasi iwapo ataendelea kuwa ndani ya jeshi la polisi.
Mji wa Ferguson pamoja
na miji mingine ya Marekani imejikuta katika ghasi na maandamano
kufuati uamuzi wa mahakama kuamua polisi huyo hapaswi kufunguliwa
mashtaka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni