Ulinzi mkali wa polisi
umewekwa leo katika eneo la Mwandoni la Kisauni, Kaunti ya Mombasa
nchini Kenya kabla ya swala ya Ijumaa.
Hatua hiyo inafutia kufungwa kwa
misikiti ya Swafaa na Minaa ambayo polisi wamedai inatumika
kuwatumbukiza vijana katika itikadi kali za kidini.
Polisi wamesema jana usiku, vijana
walijaribu kuingia kwenye msikiti Swafaa kwa ajili ya swala ya saa
mbili usiku, lakini walidhibitiwa na maafisa usalama.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni