.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

VITENDO VYA KUWATOA KAFARA WATOTO NCHINI UGANDA VYAONGEZEKA

Vitendo vya ukatili wa kutisha vya kuwatoa kafara watoto vikihusisha kuwakata viungo vyao na kupelekea vifo watoto vimezidi kushika kasi nchini Uganda.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2013 ya watoto waliotolewa kafara na kukatwa viungo Uganda inaonyesha kumekuwa na kitendo kimoja cha kumtoa kafara mtoto kila wiki, ikilinganishwa matukio saba ya kuwatoa kafara watoto yaliyoripotiwa polisi katika mwaka 2011.

Utoaji kafara watoto hao unahusishwa na masuala ya kiuchumi na mila za Uganda na hufanywa maganga wa kienyeji, mawakala wao na wateja kwa iamani viungo vyao ni dawa yenye nguvu inayotibu magonjwa yote na kutoa ufumbuzi wa matatizo mengi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni