.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

MAANDAMANO YAZIDI KUSAMBAA MAREKANI KUPINGA KUTOSHTAKIWA POLISI ALIYEUA

Makundi ya watu yameandamana katika maeneo mbalimbali nchini Marekani kupinga uamuzi wa mahakama kutomfungulia mashtaka afisa polisi aliyemuua kijana mweusi Michael Brown kwa kumpiga risasi.

Maandamano kuanzia Jijini New York hadi Seattle yalikuwa ya amani, huku waandamanaji wakipaza sauti zao na kupeperusha mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Katika kitongoji cha St Louis eneo la Ferguson, ambapo vurugu zilitawala siku ya jumatatu, jumla ya askari polisi 22,000 wamesambwazwa katika kudhibiti kutokea machafuko makubwa zaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni