.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

SERIKALI YA KENYA YAGOMA KUWAONDOA WATUMISHI WA UMMA WALIOPO MANDERA

Serikali ya Kenya imekataa kuwaondoa makumi ya maafisa wa umma pamoja na familia zao walioweka kambi katika uwanja wa ndege wa jeshi, wakiwa na mali zao baada ya kutokea tukio la kuuwawa wenzao 28 na kundi la al-Shabaab siku ya jumamosi huko Mandera.

Badala yake serikali ya Kenya, imewataka wafanyakazi hao kurejea kazini, na kuwahakikishia kuwa usalama wao utalindwa.

Hata hivyo watumishi hao wa umma wameendelea kushikilia msimamo wake kuwa wanahofia usalama wa maisha yao na kamwe hawataondoka katika eneo hilo la jeshi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni