.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

WAZIKA MAITI WATIMULIWA KAZI SIERRA LEONE BAADA YA KUTUPA OVYO MIILI YA WALIOKUFA KWA EBOLA

Watumishi wa kuzika maiti mashariki mwa Sierra Leone wamefukuzwa kazi baada ya kupora miili ya watu waliokufa kwa Ebola katika chumba cha maiti, na kuitupa maiti zake kwenye barabara kutokana na mgogoro wa malipo yao.

Watumishi hao waliokuwa katika mgomo wa siku moja kudai kutolipwa posho za kufanyakazi katika mazingira hatarishi, walitawanya makumi ya miili hiyo kuzunguka hospitali katika Mji wa Kenema.

Maiti za watu waliokufa kwa Ebola pia ziliachwa mbele ya ofisi ya meneja wa hospitali hiyo kwa mujibu maafisa wa hospitali hiyo ingawa haikuelezwa ni kwa muda gani miili hiyo iliachwa ikitapakaa kwenye hospitali hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni