.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Novemba 2014

WAUAJI WA WATU 28 KENYA WALISHANGILIA KWA KUFYATUA RISASI HEWANI BAADA YA KUTENDA UNYAMA

Imeelezwa kuwa watu wenye silaha walifyatua risasi hewani hovyo kwa furaha baada ya kuwauwa watu 28 nchini Kenya ambao inasaidikiwa si waislam katika shambulio lililotokea jana Arabiya eneo la Mandera katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Mmoja wa abiria aliyekuwemo kwenye basi lililoshambuliwa na wapiganaji hao wanaosaidikiwa ni wa kundi la al Shabaab, amesema watu hao waliokuwa wamefunika nyuso zao walifyatua risasi hizo wakiwa a sialaha nzito kama G3 na AK47, vile vile walitumia SMG na bastola.

Abiria huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama amesema wavamizi hao walikuwa wanaongea lugha za Kiswahili, Kingereza pamoja na Kisomali, na walikuwa wamevalia mavazi ya kijeshi.

Amesema kuwa walipofika eneo la Arabiya, wavamizi hao wapatao sita wakiwa wameshehena silaha walilisimamisha basi hilo, huku mmoja wao akiwa na kombora la roketi, ambapo walifyatua risasi upande wa kushoto mwa basi kabla ya kuingia ndani na kutekeleza unyama huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni