.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Desemba 2014

BALOZI SEIF AWATEMBELEA NA KUWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WAZEE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Asili wa Ijumaa Micheweni Mjini Sheikh Haji Khatib Haji.
Balozi Seif akitoa Mkono wa Pole kwa Watoto na Wajukuu wa Muasisi wa Afro Shirazy Party Marehemu Bibi Ashura Abeid hapo Nyumbani kwa Tibirinzi Chake chake Pemba.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mzee Khamis Mkadara Khamis wakati alipokwenda kumkagua na kumtakia kheir ya Mwaka Mpya wa 2015.
Mzee Bakari Khamis Kombo wa Kijiji cha Micheweni akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kumjulia hali na kumtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015.
Balozi Seif akimsalimia mzee Khamis Othman Kapona wa Kijiji cha Chekea Mtambwe alipokwenda kumtembelea na kujua hali yake pamoja na kumpa kheri ya mwaka mpya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jimbo la Micheweni Mzee Kombo Fundi Kombo wakati alipomtembelea na kujua hali yake.
                                                                     
                                                                  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara maalum ya kuwakagua baadhi ya wazee katika sehemu mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba ili kujua haliu zao pamoja na kuwapa mkono wa pongezi kwa kukamilisha mwaka 2014 na kuwatakia kheri ya mwaka mpya wa 2015.

                                                                                 Othman Khamis Ame
                                                             Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni