BENKI ya CRDB na imetiliana saini mkataba na Chama cha
Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Huduma na Biashara (TUICO) wa
kuboresha hali bora za wafanyakazi wa benki hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema mafanikio yoyote ya kibiashara
hayapatikani kama wafanyakazi ambao ndio wazalishaji hwatakuwa na mazingira
yenye maslahi bora na motisha mbalimbali.
Dk. Kimei alisema nia ya CRDB ni kuboresha mahusiano kati ya
mwajiri na wafanyakazi, kuboresha mazingiraya utendaji kazi ili kuchochea
ufanisi, kurasimisha mahusiano kati ya benki na wafanyakazi kwa kuweka miongozo
itakayosaidia kupunguza mifarakano kati ya CRDB na wafanyakazi.
“Mkataba huu ni wa miaka mitatu, utasaidia kuajiri na
uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, kushughulikia migogoro ya kikazi,
uhamisho wa viongozi wa chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi,utaratibu wa likizo
ya uzazi, likizo ya ugonjwa, ulipwaji gharama ya usafirishaji mizigo kwa
wafanyakazi wanaohamishwa, mazishi ya wazazi wa wafanyakazi, bima na utoaji
tuzo,”alisema
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni