Manchester United ni kama wameibuka kwa kasi kubwa na kuanza harakati zao za kutaka kulipigania kombe la ligi kuu ama kubakia nne bora mwishoni mwa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza, baada ya usiku wa kuamkia leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhid ya Stoke City katika mechi ya ligi kuu iliyokuwa na ushindani mkali.
Katika mchezo huo, Manchester United ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao kupitia kwa Marouane Fellaini katika dakika ya 21 ya mchezo huo.
Hata hivyo kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Stoke wajitutumue na kusawazisha katika dakika ya 39 mfungaji akiwa ni Steven Nzonzi.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Kipindi cha pili Man U walipata bao la pili mfungaji akiwa na Juan Mata katika dakika ya 59.
Kwa matokeo hayo Manchester United wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 25. Chelsea ndio wanaongoza ligi wakiwa na pointi 33, wanafuatiwa na Manchester City wenye pointi 27 na nafasi ya tatu wapo Southampton wenye pointi 26.
Michezo mingine iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ni kama ifuatavyo:-
Burnley 1 vs 1 Newcastle
Swansea 2 vs 0 QPR
Crystal Palace 0 vs 1 Aston Villa
West Brom 1 vs 2 West Ham


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni