.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Desemba 2014

FEDHA ZA ESCROW ZA MOTO, PROF. ANNA TIBAIJUKA AVULIWA UWAZIRI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete amemuachisha kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka kutokana na tuhuma za kupata mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi cha bilioni Moja na Milioni Mia Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa ajili ya shule za Sekondari ya Wasichana ya Barbro ya Jijini Dar es Salaam pamoja na Shule ya Wasichana ya Kajumulo ya Mjini Bukoba. 

Akiongea na Watanzania kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Jakaya amesema 

"tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili tuchague mtu mwingine wa kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali magumu.

Akiwa kama Mtumishi wa serikali ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi wa umma aliamua kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali haitakiwi, alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo Eliackhim Maswi amesema ameagiza uchunguzi ufanyika na katika muda wa siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni