Jenerali Alzate akiwa amezungukwa na familia yake
Jenerali wa Jeshi la Colombia Ruben
Dario Alzate, aliyeachiwa huru na waasi wa FARC siku ya jumapili
amejiuzulu wadhifa wake jeshini.
Jenerali Alzate akiwa na ulinzi
mdogo alitekwa akiwa anasafiri kwa boti kwenye ukanda wa misitu eneo
la kando ya nchi hiyo wiki mbili zilizopita.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos
ametaka kupatiwa maelezo kutoka jeshini juu ya inawezekana vipi
jenerali wa jeshi akatekwa na waasi.
Jenerali Alzate amekiri kuwa
alikiuka kanuni za kuzingatia usalama wake wakati akikatiza na boti
katika eneo alilotekwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni