.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Desemba 2014

WACHIMBAJI KOKOTO 36 NCHINI KENYA WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKA KAUNTI YA MANDERA


Wachimbaji kokoto wapatao 36 wameuwawa hii leo nchini Kenya na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab katika shambulio lililofanyika eneo la Koromei katika kaunti ya Mandera.

Wachimba kokoto hao walishambuliwa wakiwa wamelala kwenye hema na kuuwawa kwa kupigwa risasi na wapiganaji hao.

Jeshi la polisi Kenya limethibitisha kutokea vifo hivyo na kuongeza kuwa hawajabaini chanzo cha mauaji hayo, ambayo yamewalenga wachimbaji kokoto wakristo tu.

Shambulio hilo limekuja saa chache tu kupita tangu kundi moja kufanya shambulio kwenye klabu moja huko Wajir na kumuua mtu mmoja na wengine 13 kujeruhiwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni