.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Desemba 2014

TUZO ZA BALLON D' OR, VITA NI KATI YA RONALDO, MESSI NA NEUER

                                                              Cristiano Ronaldo ( mwenye jezi nyeupe )
                                                                                    Lionel Messi ( mbele )
                                                                                          Manuel Neuer.

Hatimaye Shirikisho la kandanda ulimwenguni ( Fifa ) limetangaza majina matatu ya wachezaji ambao watawania tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka 2014/2015. 

Katika majina hayo, yupo mshambuliaji mahiri wa timu ya soka ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye aliitwaa tuzo hiyo mwaka jana. 

Ronaldo atapambana na mshambuliaji hatari wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi. 

Pia mlinda mlango mahiri wa timu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer ameingia katika hatua hiyo ya fainali ya kuwania tuzo hiyo ambayo itatolewa January 12' 2015 mjini Zurich, Uswisi. 

Tujikumbushe waliopata kutwaa tuzo hii miaka iliyopita:-

2013 - Cristiano Ronaldo

2012 - Lionel Messi

2011 - Lionel Messi

2010 - Lionel Messi

2009 - Lionel Messi

2008 - Cristiano Ronaldo

2007 - Kaka

2006 - Fabio Cannavaro

2005 - Ronaldinho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni