Wanahabri wakichukua taarifa
Dotto Mwaibale
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema Mahakama isitumiwe kama kinga ya kufanya uhalifu.
Hayo yamebainishwa Dar es saalam leo na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya Sera wa LHRC, Halord Sungusia wakati akizungumza na wanahabari alipokuwa akitoa tathmini ya mwenendo wa Bunge la Tanzania katika kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
“Mahakama ni taasisi kuu kitaifa ya kutoa haki kwa wananchi wote lakini isitumiwe na mtu au taasisi yoyote kama kinga yake ya kufanya uhalifu” alisema Sungusia.
Aidha alibainisha kuwa katiba ya sasa inatoa mianya mingi ya kutozingatiwa kwa miiko ya uongozi hasa baada ya kufutwa kwa azimio la Arusha na rasimu ya pili ya katiba iliweka msingi huu wa maadili ya uongozi kwa upana na kwa msisitizo.
Sungusia aliongeza kuwa nchi haitokuwa salama kama katiba inayopendekezwa itapitishwa kama ilivyo kuwa kwani inayopendekezwa haizungumzii kwa mapana maadili na miiko ya viongozi wa umma, haiweki misingi bora ya uwajibikaji na kusimamia dhamana ya uongozi na kanuni za uongozi wa umma.
Katika hatua nyingine LHRC kimetaka wale wote ambao watabainika katika sakata la utoaji wa fedha katika akaunti hiyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni