.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Desemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA LIVERPOOL YAZINDUKA, YAITANDIKA LEICESTER 3-1

Timu ya soka ya Liverpool usiku wa kuamkia leo imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao Leicester City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza. 

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa King Power, wenyeji Leicester ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao la kuongoza kupitia kwa Leonardo Ulloa.
Kuingia kwa bao hilo kuliamsha mashambulizi kwa pande zote mbili. Hata hivyo kibao kiligeuka pale Liverpool walipoanza kuandika bao moja baada ya jingine kupitia kwa wachezaji wake, Adam Lallana, Steven Gerald na Jordan Henderson na kufanya matokeo kuwa 3-1. 

Kwa matokeo hayo, Liverpool imepanda hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 20, huku Leicester ikiwa katika nafasi ya mwisho na pointi 10.
Mwamuzi wa mchezo huo, Lee Mason akimzawadia kadi nyekundi beki wa Leicester City, Wes Morgan baada ya kumuangusha mchezaji wa Liverpool, Lambert.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni