Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera, Bw. Ashwin Rana akiwakaribisha wageni kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchini. Anayesalimiana naye ni Prof.
Longinus Rutasitara (Naibu Katibu Mtendaji Uchumi Jumla). Katikati ni
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya
kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa
na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bw. Senya Tuni.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha
ya pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Nyuma ni
shehena ya sukari iliyo tayari kuingia sokoni.
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Kiwanja cha Sukari cha Kagera
kimeanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la
sukari nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la
upatikanaji wa sukari Tanzania na nchi za jirani zinazotumia sukari
kutoka kiwandani hapo.
Hayo yamewekwa wazi na Meneja Mkuu
wa Kiwanda hicho, Bw. Ashwin Rana, wakati alipokuwa akizungumza na
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango.
“Kwa sasa tumeweza kuongeza mauzo
katika kanda kufikia tani 40,000, pamoja na kuongeza ununuzi kutoka
kwa wakulima wa miwa wa nje zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka,”
alisema.
Bw. Rana aliongeza kuwa Kiwanda
chake kimewekeza zaidi katika upanuzi wa eneo la shamba la miwa la
umwagiliaji la hekta 3600 pamoja na kuwekeza zaidi katika teknolojia
ya kisasa katika kilimo.
“Kampuni yetu imewekeza kwa kiasi
kikubwa katika teknolojia na vifaa vya kisasa ikiwemo matrekta
yanayotumia setalaiti katika ufanyaji kazi wake katika kuandaa
mashamba,” aliongeza.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri amekipongeza Kiwanda hicho kwa kuwekeza kwenye
uzalishaji wa kisasa wa miwa hali inayoongeza uzalishaji wa sukari
kuwa mkubwa kiwandani hapo.
Bibi Mwanri ameongeza kuwa Kiwanda
hicho kinastahili pongezi za kipekee kwa kuweza kuongeza ajira zaidi
ya watu 6000 waliopo kiwandani.
“Kwa kweli munastahili sifa kwa
kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania pamoja na kuuza umeme kwenye
gridi ya Taifa,” alisema.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanda
hicho, kwa sasa kinakabiliwa na na changamoto za uuzaji haramu wa
sukari zinazoingia kimagendo nchini ambao umechangiwa kushindwa kwa
kiwanda kuuza sukari ili kurudisha gharama za uzalishaji kutokana bei
za sukari zinazoagiwa kutoka nje kuwa bei ya chini sana.
“Bei ya Sukari Duniani imeshuka
sana kutokana na Nchi kubwa duniani kusaidia wakulima katika
uzalishaji na pembejeo (subsidies) na hivyo sukari kuuzwa katika soko
la dunia kwa bei ya chini (Dumping) na kufanya kuwa bei kuwa ndogo
kuliko gharama halisi ya uzalishaji,” aliongeza.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine
ni pamoja na kiwanda kushindwa kulipa mikopo iliyochokuwa benki
kutokana na kuwepo sokoni kwa sukari ambayo ni ya magendo na bei ya
chini hivyo kiwanda kushindwa kufikia malengo hata ya kiundeshaji na
mipango mikakati.
Kiwanda cha Sukari cha Kagera kiko
katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa
Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi
mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa
masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati
na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa mashine
ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu kama Centre Pivot
System.
Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine mpya
zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.
Msimamizi Mkuu wa Mtambo wa maji wa
Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul Adinani (Kulia) akitoa
maelekezo ya namna ya maji yanavyochujwa kabla ya kutumika kwa ajili
ya umwagiliaji wa miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu wa uchongaji na
usawazishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa, Mhandisi Ali
Khamis (Kulia) akitoa maelezo ya namna matrekta yanayotumia setalaiti
(hayapo pichani) yanavyofanya kazi. Wanaomskiliza ni Prof. Longinus
Rutasitara (Kushoto) ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughilikia
masuala ya Uchumi Jumla na Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa kwa
vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha shamba kwa ajili
ya uzalishaji miwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni