.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Desemba 2014

KOCHA WA MANCHESTER UNITED LOUIS VAN GAAL ASEMA KIKOSI CHAKE HAKINA HISIA ZA MAUAJI

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amekishutumu kikosi chake kwa kukosa hisia za mauaji zitakazowawezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Aston Villa.

Mchezaji Radamel Falcao alianza katika mchezo huo tangu aichezee Manchester United mapema mwezi Oktoba, na aliweza kupachika bao wavuni katika kipindi cha pili na kuisaidia United kusawazisha bao, baada ya kuwa nyuma kufuatia bao la Christian Benteke.

Manchester United iliyokuwa na rekodi ya kushinda mfululizo mechi zake sita za nyuma, ilishindwa kupata ushindi hata pale mchezaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor, alipotolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 65.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni