Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya David Kimaiyo (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph Ole Lenku (kulia).Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku na Mkuu wa jeshi la polisi nchini humo, David Kimaiyo wamejiuzulu nyadhifa zao kufuatia tukio la kuuawa kwa wachimba kokoto 36 leo asubuhi katika mkoa wa Mandera uliopo mpakani na Somalia na wafuasi wa kundi la Al-Shaabab.
Kujiuzulu kwa Ole Lenku na Kimaiyo, pia kunafuatia matukio mbalimbali ya uhalifu nchini humo ambAyo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi.
Ramani inayouonyesha mkoa wa Mandera uliopo mpakani na Somalia
Miili ya wachimbaji kokoto waliouawa mapema leo asubuhi na wafuasi wa kundi la Al-Shaabab ikiwa imelala chini baada ya kupigwa risasi.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni