.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 4 Desemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA CHELSEA HAIKAMATIKI, YAIFUMUA TOTTENHAM 3-0

 Vinara wa ligi kuu nchini Uingereza, matajiri wa London Chelsea usiku wa kuamkia leo wameendelea kuthihirisha ubora wao uwanjani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhdi ya Tottenham katika mchezo wa ligi kuu nchini humo, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
 Chelsea ambao mpaka sasa ndio wanaongoza ligi wakiwa na pointi 36 na wakiwa hawajafungwa hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi hiyo, walijipatia mabao yake kupitia kwa wachezaji wake Eden Hazard katika dakika ya 19 ya mchezo, bao la pili likifungwa na mkongwe Didier Drogba katika dakika ya 22.
Bao la tatu la Chelsea liliwekwa kimiani na mshambuliji Loic Remy katika dakika ya 73. 

Kwa matokeo hayo, Chelsea wameendelea kuwa kileleni huku wakifuatwa kwa karibu na mabingwa watetezi Manchester City.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni