.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 4 Desemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA, MANCHESTER CITY YAIZAMISHA SUNDERLAND KWA MABAO 4-1

Manchester City imeibuka na ushindi mkubwa dhidi ya wenyeji wao Sunderland wa mabao 41 katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza ambao umechezwa usiku wa kuamkia leo. 

Ikcheza ugenini, mabingwa hao watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza walijipatia mabao yao kupitia kwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa uwanjani Sergio Aguero ambaye aliifungia timu yake mabao mawili katika dakika za 21 na 71. 

Bao la pili la Manchester City lilifungwa na Stevan Jovetic katika dakika ya 39 na bao la tatu likawekwa kimiani na Pablo Zabaleta 55.
Hata hivyo katika mchezo huo, wenyeji Sunderland ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 19 ya mchezo mfungaji akiwa ni Connor Wickham. 

Kwa matokeo hayo Manchester City wamefikisha pointi 30 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni