Aidha
Mashinga aliwasihii sana wana Ihale kuweza kutumia nafasi hii ya kipekee kwao,
hivyo aliwaambia mara baada ya kumalizana na wavuvi watahamia katika sekta
nyingine na lengo likiwa ni kuwakwamua katika janga la umasikini.
Upande wa
wananchi wa Ihali waliojitokeza kwa wingi kuweza kujiunga na huduma hizo za
kijamii wakisemewa na Bw, Dionis Kabati anasema kuwa wao kama wavuvi
wanaishukuru Nssf kwa kuweza kutambua kero zao na hata kupata elimu ya kuwa kuna
mambo kama hayo ambayo sisi tulikuwa atuyajui kabisa, Hivyo aliwata viongozi
hao wa Nssf kuwa nao karibu zaidi ili waweze kubadilisha maisha yao.
Mwenyekiti
wa BMU katika mwalo wa Ihale Bw, Pius mazima anasema kuwa sasa ni wakati
mwafaka wa wavuvi kujikwamua na kwa hili hata uvuvi harama utakuwa kikomo
nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni