.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Desemba 2014

MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HEKOPTA DAR ES SALAAM


Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam, wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014. Habari na picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
               Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
 Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.
Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
                                                                                            Heshima zikiendelea…
 
Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni