Maafisa wa nchini Indonesia wamepata
miili 40 bahari wakati wakitafuta ndege ya AirAsia namba QZ8501,
iliyotoweka tangu siku ya jumapili.
Mabaki ya ndege ikiwemo miili hiyo
vimeonekana kuelea kwenye bahari ya Java, eneo la kando la Indonesia
la Borneo, ambalo ni miongoni mwa maeneo yanayotafutwa ndege hiyo.
Hata hivyo hakuna taarifa rasmi
iliyothibitisha miili hiyo imetoka katika ndege hiyo iliyotoweka.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,
ikiwa na abiria 162 wakitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea
Singapore, ilipotea siku ya jumapili.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni