.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Desemba 2014

MWANAUME MMOJA MWENYE SILAHA AUWA POLISI WAWILI NA YEYE KUJIUA

Mwanaume mmoja mwenye silaha amewapiga risasi na kuwauwa maafisa polisi wawili, walikokuwa kwenye gari la doria Jijini New York nchini Marekani, kabla na yeye kujiua pia.

Mkuu wa Polisi Jijini New York amesema mwanaume huyo alinuia kuua polisi, na baada ya kufanya hivyo alikimbilia kwenye njia ya reli ya aridhini na kisha kujipiga risasi.

Mapema mwanaume huyo alimpiga risasi na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani, na kisha kutuma ujumbe wa chuki dhidi ya polisi kwenye mitandao ya jamii.

Rais Barack Obama, ambaye yupo katika mapumziko ya Sikukuu huko Hawaii, amelaani mauaji ya polisi hao.
    Silaha iliyotumika kuwauwa polisi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni