.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 1 Desemba 2014

POLISI HONG KONG WAPAMBANA NA WANAHARAKATI WA DEMOKRASIA

Polisi Hong Kong wamepambana na wanaharakati wa demokrasia waliojaribu kulizunguka jengo la ofisi za serikali, katika machafuka mabaya kuwahi kutokea ndani ya miezi miwili ya maandamano.

Waandamanaji wamepambana na polisi wenye silaha na mabomu ya machozi ya pilipili katika barabara kwenye Wilaya ya kiutawala.

Polisi wanasema watu 40 wamekamatwa pamoja na idadi kadhaa ya maafisa polisi kujeruhiwa katika mapambano hayo.

Waandamanaji wanataka watu wa Hong Kong kuruhusiwa kuchagua viongozi wao katika uchaguzi wa mwaka 2017 bila ya kuingiliwa na Beijing. 
                                        Polisi akimchapa mjeledi mmoja wa waandamanaji

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni