Rais Barack Obama wa Marekani
ameomba kiasi cha dola milioni 263 kuboresha mafunzo ya polisi,
kununulia kamera ya kuvaa mwilini na kurejesha imani kwa jeshi la
polisi.
Rais Obama ameliomba baraza la
Congress fedha hiyo baada ya kuwepo maandamano ya kitaifa ya wiki
moja kushutumu jeshi la polisi kutowatendea haki watu weusi.
Mji wa Ferguson eneo la Missouri
ulikumbwa na machafuko baada ya mahakama kuamua kutomfungulia
mashtaka polisi mzungu aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi
asiyena silaha.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni