.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Desemba 2014

REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA DUNIA KWA VILABU

Real Madrid wameshinda kombe lao la tano kwa mwaka 2014, baada ya kuwafungwa mabingwa wa Amerika ya Kusini timu ya San Lorenzo na kutwaa Kombe la Dunia kwa vilabu, katika fainali iliyofanyika Morocco.

Katika mchezo huo mabingwa hao wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Mabingwa wa Kombe la Copa del Rey na Kombe la Super la Ulaya, walipata bao la kuongoza kupitia Sergio Ramos aliyeutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa.

Makosa ya golikipa wa San Lorenzo yaliiwezesha Real Madrid kupata bao la pili kupitia kwa winga wake mwenye kasi Gareth Bale, katika michezo huo ambao hadi mwisho matokeo yalikuwa Real Madrid 2-0 San Lorenzo.
                                              Wachezaji wa Real Madrid wakifurahi ushindi


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni