.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Desemba 2014

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MADEREVA SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)

SHIRIKA la Usafiri Dar es Salaam (UDA) linawatangazia Watanzania wote hususan wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba linahitaji kuajiri madereva kwa ajili ya kuendesha mabasi yake hapa jijini.

                                                                            SIFA ZA WAOMBAJI

Waombaji wa kazi ya udereva wanatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30-55, ujuzi wa udereva wa mabasi kutoka katika vyuo vya VETA, NIT, au chuo kingine kinachotambulika na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi nchini (NECTA). Pia wanapaswa kuwa na leseni ya udereva daraja C Kavu (Class C Plain) na daraja C1(Class C1) , rekodi nzuri ya utendaji na afya njema.

                                                                          NAMNA YA KUOMBA

Waombaji wote walete barua zao za maombi wakiambatanisha na barua za udhamini, walete barua hizo kwa mkono katika Ofisi ya Afisa Rasilimali watu na Utawala, Makao Makuu ya UDA, KAMATA COMPLEX, mahali zilipokuwa ofisi za mabasi ya SCANDINAVIA.

                                                 Wanawake wanyesifa wanahimizwa zaidi.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA 255222127421, 0766777754, 0766777753 ,0754776700, 0715776500,0712000037 au wasiliana kwa barua pepe info@uda.co.tz, uda@umojainvestments.com au kwa sanduku la posta 


                                                       Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) 
                                                         
                                                                                        S.L.P 872 

                                                                     Dar Es Salaam,Tanzania

LIMETOLEWA NA OFISI YA MAHUSIANO YA UMMA UDA

DESEMBA 01, 2014.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni