Kura zinaendelea kupigwa katika
uchaguzi nchini Liberia ambao ulilazimika kuhairishwa mwezi Oktoba
kutokana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola.
Katika uchaguzi huo wananchi wa
Liberia wanawachagua wawakilishi wao katika baraza la Seneti.
Miongoni mwa wagombea 139 wanaowania
nafasi 15 za Useneta yupo mwanasoka nyota wa zamani wa nchi hiyo
George Weah pamoja na Robert Sirleaf, ambaye ni mtoto wa kiume wa
rais wa Liberia.
Ugonjwa wa Ebola uliambukiza watu
19,000 katika nchi za Afrika Magharibi na kuuwa watu zaidi ya 7,373,
huku vifo 3,346 vikitokea Liberia kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa
Mataifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni